Libya iliwekewa vikwazo vya fedha mwanzoni mwa mwaka huu wakati harakati za mapinduzi zilipopamba moto nchini humo ili kumdhibiti kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.Katika upande mwingine Baraza la Taifa la Mpito la Libya limezitaka nchi zote duniani kuirejeshea Libya fedha zake zilizozuiliwa wakati wa uongozi wa Kanali Muammar Gaddafi.Mustapha Abdul Jalil Mkuu wa baraza hilo ameitaka jamii ya kimataifa kuachilia fedha zilizozuiliwa za Libya ili zitumike kwa ajili ya maendeleo ya nchi hiyo.Abdul Jalil amesema kuwa fedha hizo zinakadiriwa kuwa kati ya dola bilioni 140 hadi 160 za Kimarekani na kuongeza kwamba taifa la Libya linahitajia fedha hizo kwa ajili ya kulipa mishahara na kuirejesha nchi hiyo katika hali ya kawaida.Hii ni katika hali ambayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema kuwa, nchi yake itairudishia Libya Euro milioni 230 ambazo ilikuwa imezizuia.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 284648
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeiondolea Benki Kuu ya Libya vikwazo pamoja na benki zake zinazowekeza nje ya nchi, hatua ambayo imechukuliwa ili kupunguza tatizo la fedha kwa nchi hiyo.